Saturday, June 18, 2016

"SINA MPANGO WA KUHAMIA SIMBA" JEBA

Kiungo Ibrahimu Jeba wa klabu ya Mtibwa Sugara amesema hana mpango wa kuihama Mtibwa Sugar kwa sasa.

Simba walionyesha nia ya kumuhitaji kiungo huyo lakini yeye mwenyewe amedai hana mpango wa kuhamia klabu hiyo, Jeba amesema anajua madhara ya kucheza timu kubwa kama Simba hivyo haoni sababu ya  kuenda huko na kuona ni bora abaki katika klabu yake ya Mtibwa ambapo anauhakika wa kucheza.

Akielezea sababu ya kwanini hapendi kucheza katika klabu kubwa Jeba alisema, Vilabu vikubwa mara nyingi huua vipaji vya wachezaji wazawa pale vinaposajili wachezaji wa kigeni huku akisisitiza kuwa mipango yeye ni kuisaidia klabu yake kupata mafanikio ikiwemo kutwaa taji la ligi kuu Vodacom.

"Nashukuru kwa timu kubwa kuonyesha imani ya kunihitaji, lakini bado sijafikiria kuondoka Mtibwa, kwa sababu ninafurahia maisha ya hapa na hata maslahi ambayo ndio kitu kikubwa katika mchezo wa soka" alima Jeba.

Bonyeza hapa ku-Like Page ya Soka24 Facebook


Related Posts:

  • AUBAMEYANG AITAMANI REAL MADRID Hakuna ubishi kuwa Nyota wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang anatamani kujiunga na miamba ya soka ya nchini Hispania klabu ya Real Madrid. Aubameyang amewahi kumuahidi babu yake kuwa ipo siku atakuja kucheza k… Read More
  • WALIOSAJILIWA,WALIOACHWA MAN U MSIMU WA 2016-17 Kuelekea Msimu wa 2016-17 klabu ya Manchester United imekamilisha Usajili Ufuatao; WALIOINGIA; MCHEZAJI KLABU ALIYOTOKA ADA YA UHAMISHO Eric Bailly … Read More
  • MAISHA YA FABREGAS CHELSEA YAFIKA UKINGONI Cesc Fabregas ameambiwa na kocha wa klabu ya Chelsea Antonio Conte kuwa anaweza kuondoka klabuni hapo. Conte ametoa kauli hiyo huku kukiwa kumebaki siku 2 tu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili barani ulaya. Kiungo h… Read More
  • WEST BROM YAVUNJA REKODI YA KLABU USAJILI WA CHADLI Klabu ya West Bromwich Albion imevunja rekodi ya klabu hiyo kwa kumsajili Winga wa Tottenham Spurs kwa kitita cha Pauni milioni 13. Chadli alijiunga na Spurs akitokea FC Twente kwa uhamisho wa pauni milioni 7 Julai 2013… Read More
  • Rasmi: Wilfred Bony Atua Stoke City Klabu ya Stoke City imekamilisha uhamisho wa Wilfred Bony kwa mkopo akitokea klabu ya Manchester City. Bony aliyefeli kumshawishi kocha mpya wa City, Mhispania Pep Guardiola amefanikiwa kufunga magoli 11 katika michezo 4… Read More

0 comments:

Post a Comment