Mwenyekiti wa Stand United, Aman Vicent amesema mpira wa miguu unaendeshwa kwa kufuatia kanuni na katiba, lakini SHIREFA inakiuka kanuni na kuandikisha wanachama pamoja na kuitisha uchaguzi.
"TFF ilitupa barua ya kututaka kuandaa uchaguzi, nakala walipeleka Shirefa na BMT (Baraza la michezo la Taifa) na sisi tuliifanyia kazi, kwani tuliunda kamati na kuituma TFF, lakini kuna watu wametangaza uchaguzi kuwa ni juni 26 kinyume na kanuni, hivyo tunaomba TFF ikemee jambo hilo" alisema Amani.
Mwenyekiti huyo alidai masuala hayo ni kutokana na timu hiyo kuwa na ufadhili na kuomba TFF iingilie kati jambo hilo, aliongeza kwa kusema Bodi ya wakurugenzi ya klabu hiyo iliyokaa hivi karibuni iliteua kamati ya uchaguzi ambayo itaongozwa na Alan Maduhu (Mwenyekiti), Denis Deogratius (Makamu Mwenyekiti) na wajume ambao ni Yusuph John, Omari Kiyungi na Ezron Mwanjelenga.
0 comments:
Post a Comment