Thursday, June 16, 2016

KIFAA KIPYA YANGA KUTUA LEO JANGWANI

Walter Musona Mshambuliaji kutoka FC Platinum ya Zimbabwe anatarajiw kuwasili Daresalaam leo alasiri kwa ajili ya mazungumzo na klabu ya Yanga.

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka katika klabu ya Yanga, tayari mambo yote muhimu kuhusiana na ujio wake yamekamilika na kuna matarajio makubwa wakafikia makubaliano na mchezaji huyo na kuanza kuitumikia Yanga msimu ujao.

"Atafika Dar Es Salaam kesho (leo), tunaamini suala lake litaisha na atakuwa mchezaji wa Yanga", kilisema chanzo hicho.

Habari zaidi zinasema dili hilo la kumleta Musona Yanga linasimamiwa kikamilifu na nyota wawili wa Zimbabwe wanaoitumikia klabu ya Yanga kwa sasa, Donald Ngoma na Thaban Kamusoko.
Musona ndiye aliwafunga Yanga goli moja kwa mpira wa adhabu ndogo wakati Yanga ilipowafunga Platinum magoli 5 - 1 uwanja wa Taifa, Dar Es Salaam mwaka jana.

Mshambuliaji huyo anauwezo wa kucheza namba 10, 8 na 6 lakini pia anaweza kucheza winga zote.

Bonyeza hapa ku-Like Page ya Soka24 Facebook

Related Posts:

  • JOHN BOCCO NJE AZAM DHIDI YA AFRICAN SPORTS NAHODHA wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’, ameingia kwenye orodha ya wachezaji majeruhi wa timu hiyo baada ya misuli yake ya mguu kukaza. Tokea jana mshambuliaji huyo amekuwa a… Read More
  • TFF YABEBESHWA LAWAMA MATOKEO MABAYA YA SIMBA SC RAIS wa Simba Sports Club Evans Aveva jana alijitokeza mbele ya waandishi wa habari akielezea hali mzima ya ligi kuu Tanzania Bara na muendelezo wa matokeo mabaya ya Simba. Katika hotuba yake Aveva ameitupia lawama TFF … Read More
  • HIZI NDO ZITAKAZOSHUKA DARAJA LIGI KUU BARA Wakati Coastal Union ya Tanga ikiwa imeaga rasmi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania 2015/16, swali linabaki kwa wadau wa soka nchini kwamba ni timu gani itaungana na Wagosi wa Kaya kushuka daraja kutokana na timu tano kuwa kat… Read More
  • KIKOSI CHA SIMBA CHAPEWA LIKIZO FUPI SIMBA iliyotoka kucheza na Mtibwa Sugar jana na kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila goli lililofungwa na Abdi Banda, imepewa mapumziko mafupi kabla ya kuanza kujiandaa na mchezo wao wa mwisho wa ligi dhidi ya JKT Ru… Read More
  • KIKOSI CHA YANGA LEO DHIDI YA NDANDA FC LIGI KUU TANZANIA BARA Ndanda SC Vs Young Africans SC  Uwanja : Taifa. Muda : Saa 10 : 00. Kikosi Cha Yanga. 1.Deogratius Munishi Dida. 2.Juma Abdul Jafary. 3.Mwinyi Haji Ngwali. 4.Vicent Bossou. 5.K… Read More

0 comments:

Post a Comment