Sunday, May 8, 2016

TAYARI MAN UTD IMENASA SAINI ZA WACHEZAJI HAWA 4


Mashabiki wa Manchester United wanahamu kubwa ya kujua kina nani watatua katika klabu yao mara baada ya kumalizika msimu huu wa Ligi kuu. Lakini wakiwa katika shauku hiyo tayari klabu ya Man UTD imeshanasa saini za makinda 4 watakaoongeza nguvu katika kikosi hicho msimu ujao.

Wachezaji hao ni: Mlinda Mlagno raia wa Nchini Poland Kacper Chorazka, straika wa FC Zurich Nishan Burkart, Forward kutoka  nchini Uholanzi Tahith Chong na Nahodha wa timu ya Taifa ya Vijana (Under 16)  ya Jamhuri ya Ireland  Lee O’Connor.

0 comments:

Post a Comment