Sunday, May 8, 2016

MALIMI BUSUNGU NJE WIKI 4



KLABU ya Yanga jana iliikaribisha Sagrada Esperanca ya nchini Angola katika mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Africa, Yanga iliibuka na ushindi wa magoli 2 - 0, yaliyofungwa na Simon Msuva na Matheo Anthony.

Katika Mchezo huo, Mshambuliaji wa Yanga Malimi Busungu hakuweza kuendelea na mchezo baada ya kugongana na kipa wa Segrada Esperanca hivyo kukimbizwa hospitali, uchunguzi wa madaktari umebaini kuwa Busungu amepata Majeraha ya mbavu na kidonda cha fuvu.
Hivyo anatazamiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki 4 akiuguza majeraha yake. 

0 comments:

Post a Comment