UEFA Champions League imeendelea tena jana kwa mechi mbili zilizozikutanisha timu za Real Madrid vs Wolfsburg na Manchester City vs PSG.
katika mechi hizo timu za Real Madrid Na Manchester City ya Uingereza zimefanikiwa kutinga katika hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo Baada ya kuziondosha klabu za PSG na Wolfsburg.katika Mchezo wa Madrid vs Wolfsburg Madrid walikuwa wanahitaji ushindi wa goli tatu kwa sufuri kufuatia kufungwa katika mchezo wao wa kwanza uliochezwa Ujerumani. Christiano Ronaldo ndiye alikuwa nyota wa mchezo huo baada ya kufanikiwa kuisaidia timu yake kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali kwa kuifungia timu yake magoli matatu ( Hat Trick ). Magoli ya Ronaldo yalipatikana katika dakika za 15', 17' na 77'
Wolfsburg walicheza vizuri lakini walikosa umakini katika umaliziaji.
Nako katika upande wa pili Manchester City wamemtoa kimasomaso kocha wao anaeondoka mwisho wa msimu wa mwaka huu baada ya Guardiola kusaini mkataba na Vijana hao wa Etihad, katika mchezo huo uliokuwa wa vuta nkuvute mshambuliaji hatari wa kiagentina Aguero alikosa penalti ,lakini makosa yake yalisahihishwa na Kevin De Bruyne aliyeifungia Manchester City goli la pekee na la ushindi dakika ya 76' .PSG walilazimika kuyaaga mashindano hayo kufuatia sare ya 2 - 2 waliyoipata katika uwanja wao wa nyumbani nchini Ufaransa.
Madrid na Man City zinakuwa timu za kwanza kufuzu kucheza hatua ya nusu Fainali huku zikizisubiri timu zitakazoshinda katika michezo ya leo ambapo Atletico Madrid watakuwa katika uwanja wake wa nyumbani kuikaribisha Barcelona huku Bayern Muchen watasafiri kuifata klabu ya Benfica.
Magoli matatu ya jana ya Christiano Ronaldo yanamfanya kuongoza chati ya wafungaji bora msimu huu akiwa ameshapachika nyavuni magoli 11 huku akifuatiwa na Robert Lewandowsk mwenye magoli 7.
0 comments:
Post a Comment