UEFA Euro 2016 inatarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni, na timu zote shiriki zimeshatangaza vikosi vyao vya wachezaji 23 watakaochuana kufukuzia kombe hilo ambalo kwa mwaka huu mashindano hayo yatafanyika nchini Ufaransa, timu 24, viwanja 10, mechi 50 katika mwezi mzima wa purukushani kupigania taji hilo,nje ya uwanja wanawake na wapenzi wa wachezaji watakuwa wakishuhudia waume zao wakiliwinda kombe hilo.
Soka24 hap
a inakuletea orodha ya warembo wa wachezaji hao ambao wataenda na waume zao kushuhudia michuano hiyo.
Ludivine Kadri Sagna- Ufaransa
Bacary Sagna amechaguliwa katika kikosi cha Ufaransa kitakachocheza michuano hiyo ya Euro 2016 na atakuwa akishuhudiwa na kipenzi chake Ludivine katika mechi zake zote.
Edurne- Hispania
David De Gea katika misimu yake aliyocheza katika klabu ya Machester United kumemfanya kuwa chagua la kwanza kwa upande wa walinda mlango wa timu ya taifa ya Hispania, na jina lake litakuwa la kwanza kutajwa katika list ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Mpenzi wake De Gea Edurne atakuwepo katika michuano hiyo kumtazama mumewe akiipigania timu yake.
Pilar Rubio-Hispania
Mmoja kati ya wanawake wenye mvuto zaidi, Pilar Rubio ni mke wa mchezaji wa Real Madrid Sergio Ramos, Ramos ambaye katika michuano hiyo atakuwa ni miongoni mwa wachezaji wazoefu zaidi.
Lena Gercke-Ujerumani
Sami Khedira anatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika kikosi cha Ujerumani katika nafasi ya kiungo, na mrembo wake Lena atakuwa jukwaani akimshangilia, alifanya hivyo pia katika michuano ya mwaka 2014.
Lena-Ujerumani
Hajaonekana kwa muda mrefu tangu michuano ya kombe la dunia lililofanyika mwaka 2014, lakini endapo Julian Draxler mpenzi wake atachaguliwa katika kikosi cha mwisho kitakachotajwa kushiriki michuano hiyo basi tutashuhudia uzuri wa binti huyo anayeitwa Lena.
Sam Cooke-England
Ni kipenzi cha mchezaji wa Manchester United Chris Smalling, Smalling ni chaguo pekee katika nafasi ya mlinzi wa kati katika klabu yake ya United lakini uwezo wake umemfanya pia kuaminiwa katika kikosi cha Uingereza. Mpenzi wake Sam Cooke anatukuwa ni miongoni mwa wanawake warembo zaidi kuwepo katika fainali hizo za euro 2016
Viktoria Varga-Italy
Graziano Pelle kwa bahati nzuri amepata nafasi ya kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Italia kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha akiwa na klabu yake ya Southampton na mpezi wake mwanamitindo Viktoria ni wa kutazamwa katika michuano hiyo.
Anna Lewandowska-Poland
Lewandowski amethibitisha ubora wake na kuwa mmoja kati ya washambuliaji hatari zaidi duniani baada ya kuonyesha kiwango kikubwa katika ligi kuu nchini Ujerumani akiwa na klabu yake ya Bayern Munich, nje ya uwanja pia Lewandowksi yuko vizuri kwani uzuri wa mke wake Anna Lewandowska unathibitisha hilo.
Natalia Ignashevich-Russia
Sergei Ignashevich anacheza katika klabu ya CSKA Moscow na ataiwakilisha Urusi katika mashindano ya Euro mwaka huu, mkewe Natalia atakuwepo katika michuano hiyo.
Renata Langmannova-Czech Republic
Langmannova anatembea na Martin Fenin wa Jamhuri ya Czech na huenda akaenda au asiende katika michuano hiyo.
Michele Lacroix-Ubelgiji
Michele Lacroix ni mpenzi wake na mchezaji wa Manchester City Kevin De Bruyn na wamekuwa pamoja muda wote tangu wakiwa wadogo.
Barbara Megert-Uswiss
Barbara ni mpenzi wake na Blerim Dzemaili mchezaji wa timu ya Taifa ya Uswizi
Elena Bonzanni-Uswiss
Elena ni kipenzi cha Mchezaji wa kimataifa wa Uswiss Velon Behrami
Alexandra ivarsdottir-Iceland
Alexandra ni mpenzi wa midfielda wa Swansea City Gylfi Sigurdsson, atakuwepo pia katika michuano hiyo ya Euro wakati timu ya taifa ya Iceland itakapokuwa inapambana kutwaa kombe hilo.
Emma Rhys-Jones-Wales
Gareth Bale mchezaji wa kutegemewa wa timu ya taifa ya Wales ataongozana na kipenzi chake Emma kuelekea Ufaransa katika uero 2016.
Tatjana Batinic-Austria
Tatjana Batinic ameshatembea na wachezaji kadhaa akiwemo Ivan Rakitic wakati akiwa FC Shalke na sasa ameolewa na Sebastian Boenisch ambae atakuwa anasafiri na timu yake ya taifa ya Austria kuelekea nchini Ufaransa.
Claudine Keane-Slovakia
Mrembo kutokana Ireland mke wa Robbie Keane Claudine Keane huenda nae akasafiri kuelekea nchini Ufaransa kushuhudia euro 2016
Barbora Lovasova-Ireland
Ni mke wa mchezaji wa Liverpool Martin Skrtel ambae ni majeruhi kwa sasa na huenda akaikosa michuano ya euro 2016.
0 comments:
Post a Comment