Saturday, May 14, 2016

SUPER MARIO AKUBALI KUJIUNGA NA MAN UNITED


Manchester United wanakaribia kumalizana na mchezaji wa Sporting Lisbon Joan Mario.
Mabosi wa United wamefanya mazungumzo mara kadhaa na mchezaji huyo mwenye miaka 23 raia wa Ureno na wakala wake anaamini dili hilo litatimia.

Mkataba wa Mario unaonyesha kuwa klabu itayohitaji kunasa saini ya mchezaji huyo inatakiwa kutoa kitita cha paundi milioni 45 na Man Utd wanaonekana  kuwa tayari kutoa kiasi hicho cha fedha na kumpa mchezaji huyo  mkataba mrefu.
Hata hivyo licha ya mkataba kuonyesha thamani ya Mario kuwa ni paundi milioni 45 Manchester watalazimika kuongeza paundi milioni 2 kutokana na mahitaji ya klabu ya Sporting.
Joan Mario

United waligeukia kwa Mario baada ya kuikosa saini ya mchezaji wa Benifica Renato Sanches ambaye amechagua kujiunga na Bayern Munich badala ya United.

0 comments:

Post a Comment