Klabu ya Simba ipo katika pilikapilika za kuhakikisha wanaimarisha kikosi chao lengo likiwa ni kutwaa ubingwa wa ligi msimu ujao.
Katika kuhakikisha wanafanya usajili wa uhakika Simba imeelekeza nguvu zake nchini Uganda, Zambia pamoja na Zimbabwe. Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alikuwa Zimbabwe hivi karibuni kwa ajili ya kusaka wachezaji.
Klabu ya Simba imekosa ubingwa kwa miaka mitatu mfululizo na sasa wanajipanga kurudi katika fomu yao na hata kutwaa ubingwa wa ligi kuu Vodacom msimu wa 2016/17.
"Nguvu Zinaelekezwa Uganda, tunamtumia kocha wetu Jackson Manyanja tunaamini tutapata wachezaji weneye uwezo wa kuisaidi Simba" alisema.
"Yapo majina ya nyota waliopo katika timu ya Taifa ya Uganda "The Cranes" lakini kwa sasa siwezi kuyasema, lakini tutashangaza wengi"
Kocha Patrick Phiri na Jackson Mayanja ndio wanaowatumia katika kuhakikisha wanawapata wachezaji wazuri ambao watakuwa chachu ya ushindi katika klabu ya Simba.
Hans Poppe alisema wanapambana huku na kule kutafuta kocha na wachezaji ambao watairudisha Simba katika kiwango chake huku akisisitiza kuwa usajili watakaoufanya mwaka huu utakuwa wa tofauti sana ukilinganishwa na usajili waliokuwa wanaufanya huko nyuma na kwamba mchezaji yoyote wa kigeni atakayesajiliwa klabuni hapo ni lazima awe anaichezea timu yake ya taifa huko kwao.
==============
Bonyeza hapa ku-Like Page yetu ya Facebook
==============
0 comments:
Post a Comment