Wednesday, June 15, 2016

USAJILI YANGA NI MWENDO MDUNDO

Klabu ya Yanga imesema bado ina mipango ya kusajili wachezaji wa kimataifa kwa ajili ya kukisaidia kikosi chao kufanya vizuri katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika (CAF CC).

Yanga imeshawanasa wachezaji wanne wa ndani ambao ni Hassan Ramadhani, Ben Kakolanya, Vicent Andrew na Juma Mahadhi. Habari za ndani ya Klabu ya Yanga zinasema mabingwa hao wa ligi kuu Bara wameshaanza mazungumzo na wachezaji wa kimataifa na kuna dalili za kuafikiana katika mazungumzo hayo na hayo yakishakamilika basi watawekwa hadharani.

Kwa sasa Yanga inawachezaji sita wa kigeni, Amis Tambwe, Haruna Niyonzima, Thabani Kamusoka, Donald Ngoma, Vicent Bossou na Issoufou Boubacar.

"Bado tuna nafasi ya kuongeza mchezaji na kwa sasa kuna mazungumzo yanaendelea na wachezaji kadhaa wa kimataifa, tukikubaliana wakati wowote watakuja kumalizana" alisema moja ya viongozi wa Yanga.

Kiongozi huyo alisema wakati wanaendelea na usajili huo, wanafikiria pia namna ya kulishawishi shirikisho la soka Tanzania TFF kuzidisha usajili wa wachezaji wa kigeni na kufikia kumi, lengo likiwa ni kupata nafasi ya kutafuta wachezaji wengi wazuri nje ya nchi.

Yanga itacheza mechi yake ya kwanza katika hatua ya makundi Jumapili Juni 19, dhidi ya MO Bejaia.

Bonyeza hapa ku-Like Page ya Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment