Wednesday, June 15, 2016

KIFAA KIPYA CHAAHIDI MAKUBWA SIMBA

Kiungo mshambuliaji aliyesajiliwa na Simba hivi karibuni Jamali Mnyate amesema kusaini kwake Simba mkataba wa miaka 2 ni kujiendeleza kimpira na kuisaidia Simba kupata mataji.


Mnyate aliyejiunga na Simba akitokea Mwadui FC, amesema Simba sio mwisho wa mafanikio yake bali ni njia nzuri kwake kama mchezaji kufikia mafanikio makubwa ya kuwa mchezaji wa kulipwa.

"Nimesaini mkataba wa miaka miwili kutimiza ndoto zangu, nilikuwa na ndoto ya kuichezea klabu kubwa nchini na Simba ni mojawapo ya timu kubwa nchini" alisema Mnyate.

Mnyate amewaahidi mashabiki wa Simba kujitolea kwa moyo wake wote ili kuisaidia timu kufanya vizuri msimu ujao na kuomba ushirikiano wao.

Jamali Mnyate ni Mzaliwa wa Kilosa, Morogoro, Agosti 7, 1992, amewahi kucheza timu za Taifa za vijana, Burkina Faso ya Morogoro, Azam Fc ya Daresalaam, Mtibwa Sugar na sasa yuko Simba SC.

Bonyeza hapa ku-Like Page ya Soka24 Facebook

Related Posts:

  • KIFAA KIPYA YANGA KUTUA LEO JANGWANIWalter Musona Mshambuliaji kutoka FC Platinum ya Zimbabwe anatarajiw kuwasili Daresalaam leo alasiri kwa ajili ya mazungumzo na klabu ya Yanga. Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka katika klabu ya Yanga, tayari mambo yo… Read More
  • HUYU NDO KOCHA MPYA BRAZILTite ametajwa kuwa kocha mpya wa Brazil baada ya Dunga kutupiwa virago kufuatia matokeo mabovu waliyoyapata Brazil Copa America 2016. Tite Tite 55, anachukua nfasi ya Dunga aliyetimuliwa mara baada ya Brazil kutolewa hatu… Read More
  • KIFAA KIPYA CHAAHIDI MAKUBWA SIMBAKiungo mshambuliaji aliyesajiliwa na Simba hivi karibuni Jamali Mnyate amesema kusaini kwake Simba mkataba wa miaka 2 ni kujiendeleza kimpira na kuisaidia Simba kupata mataji. Mnyate aliyejiunga na Simba akitokea Mwadui F… Read More
  • USAJILI YANGA NI MWENDO MDUNDOKlabu ya Yanga imesema bado ina mipango ya kusajili wachezaji wa kimataifa kwa ajili ya kukisaidia kikosi chao kufanya vizuri katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika (CAF CC). Yanga imeshawanasa wachezaji wann… Read More
  • MATARAJIO YA SIMBA KIKOSI KIPYA MSIMU UJAOZacharia Hans Poppe, mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba, amesem a kikosi chao msimu ujao kitakuwa na mabadiliko makubwa kuanzia benchi la ufundi hadi wachezaji. Simba kwa sasa ipo katika harakati za kuhakikisha wanawana… Read More

0 comments:

Post a Comment