Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeingia kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana.
Serengeti Boys iliingia kambini jana chini ya kocha Bakari Shime, na itashuka dimbani Juni 26 kumenyana na Shelisheli, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na zitarudiana wiki moja baadaye nchini Shelisheli.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alitaja kikosi ambacho kimeingia kambini kinaongozwa na makipa Kelvin Kayego, Ramadhan Kambwili na Samweli Brazio.
Mabeki ni Kibwana Shomari, Israel Mwenda, Anton Makunga, Nickson Kibabage, Dickson Job, Ally Msengi na Issa Makamba. Aliwataja viungo ni Kelvin Naftal, Ally Ng’anzi, Shabani Ada, Mustapha Mwendo, Yassin Mohamed, Syprian Mtesiwa na Gadaf Said.
Wengine ni Asad Juma, Mohamed Rashid na Muhsin Makame huku washambuliaji ni Ibahim Ally, Enric Nkosi, Rashid Chambo na Yohana Mkomola.
Bonyeza hapa ku-Like Page ya Soka24 Facebook
0 comments:
Post a Comment