Saturday, May 14, 2016

NDANDA FC WAPANIA KUHARIBU SHEREHE YA YANGA


Msemaji wa klabu ya Ndanda FC Idrisa Bandari amesema watahakikisha wanaifunga Yanga na kuharibu Sherehe yao ya kukabidhiwa kombe leo katika mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar.
Yanga wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa tayari mabingwa huku mchezo huo ukiambatana na sherehe za kukabidhiwa kombe la ligi kuu Bara msimu wa 2015/16, 

Bandari amesema kwao wao mchezo wa leo una umuhimu mkubwa huku wakitaka kutoka katika nafasi waliyopo katika msimamo wa ligi na kusogea katika nafasi za juu zaidi, akizungumza jana Idrisa amedai kikosi cha Ndanda kimejiandaa vizuri na kipo tayari kuwavaa Mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania Bara mara 26.

Kwa upande mwingine afisa habari wa Yanga, Jerry Muro amesema wao hawauchukulii mchezo huo kama bonanza bali mchezo ambao wanahitaji kushinda ili kuweka heshima zaidi katika ligi kuu Bara, akizungumza kwa majigambo Muro amesema Yanga ni Wakimataifa na wanataka kulithibitisha hilo pia kwa kushinda mechi ya leo, aliendelea kwa kusema sio ajabu kwa mashabiki watakao hudhuria leo uwanjani wakamuona Donald Ngoma akikaa golini badala ya kucheza ndani huku Ally Mustafa na Deogratius Munish wakicheza ndani kwani wote ni wachezaji na ni katika kuuthibitishia umma kuwa Yanga inaweza na kwamba inaweza pia kufanya kitu chochote katika mpira.

Tayari TFF wameshatangaza kuwa Waziri wa Kilimo, Ufugaji na Uvuvi Mwigulu Nchema ndiye atakaekabidhi kombe hilo kwa vijana wa Jangwani katika sherehe hizo zitakazofanyika baada ya mechi kumalizika, Yanga pia wanatarajia kusafiri kwenda Angola kucheza mechi ya marudiano hatua ya mtoano kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya GD Sagrada Esperanca.

0 comments:

Post a Comment