Michezo kadhaa kupigwa jumapili hii kote duniani tukianzia
nyumbani Tanzania ligi kuu Tanzania Bara kuendelea katika viwanja vinne vya
miji tofauti.
Macho ya wapenda michezo wengi Afrika mashariki yapo uwanja
wa Uhuru ambapo utafanyika mchezo namba 76 utakao zikutanisha Azam matajiri
hawa wa jiji na mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga, ikumbukwe kua Yanga na Azam
wanapokutana Hakuna kuoneana haya kwani
hua huwezi kutabiri ni nani ataibuka mshindi wa mchezo. Mchezo huo wa leo jioni
majira ya saa kumi utachezeshwa na mwamuzi Israel Nkongo wa Dar es Salaam. Nkongo atasaidiwa na Soud
Lila na Frank Komba na mwamuzi wa akiba atakuwa Helen Mduma; wote wa Dar es
Salaam. Kamishna wa mchezo atakuwa Michael Wambura pia wa Dar es Salaam.
Mchezo mwingine ni mchezo namba 77 utakaopigwa dimba la
Mabatini Mlandizi Pwani wakati wenyeji Ruvu Shooting ya Pwani zidi ya timu ya
jiji la Mbeya Mbeya city mchezo utakaochezeshwa na mwamuzi Rudovic Charles wa Tabora akisaidiwa na Samwel
Mpenzu wa Arusha na Jeremina Simon wa Dar es Salaam.Kamisha wa mchezo huo
atakuwa Idelfonce Magali wa Morogoro.
Mchezo mwingine utazikutanisha Mtibwa sugar ambayo inakumbukumbu
ya kipigo cha goli 3 kwa 1 kutoka kwa Yanga katikati ya wiki wataikaribisha
Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo namba 78 ambao utachezeshwa na mwamuzi Elly Sasii wa Dar es Salaam. Waamuzi wasaidizi
ni Ferdinand Chacha wa Mwanza Lulu Mushi wa Dar s Salaam wakati mwamuzi wa
akiba Nicolaus Makalanga wa Morogoro. Kamishna ni George Komba wa Dodoma.
Mchezo mwingine ni ule
wenye namba 78 kati ya wenyeji wa mkoa wa mwanzaToto African ya Majimaji ya
Songea kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mchezo huo utasimamiwa na mwamuzi Shomary
Lawi wa Kagera akisaidiwa na Abdallah Uhako wa Arusha na Julius Kasitu wa Shinyanga
huku mwamuzi wa akiba akiwa Mathew Akrama wa Mwanza. Kamishna atakuwa Michael
Bundala wa Dar es Salaam.
Ratiba hii ni
kwa msaada wa Tff
Michezo yote
itapigwa saa kumi kamili jioni
0 comments:
Post a Comment