Sunday, October 16, 2016

MATOKEO YA MICHEZO YA LEO VPL


MATOKEO YA MICHEZO YA LEO VPL
Uwanja wa uhuru tumeshuhudia mpira ukiwa ni wa kupaniana sana hasa kipindi cha kwanza ambapo kadi za njano nyingi zilitoka na huku kila timu ikionekana kutokumwamini mwamuzi Israel Nkongo. Mpka kipindi cha kwanza kinakamilika timu zilitoka sare tasa na kushuhudia Juma Abdul akitolewa baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Mbuyu Twite.
Kipindi cha pili Azam waliachana na mwamuzi na kuanza kujiamini na kutengeneza nafasi nyingi lakini umakini wa beki wa yanga na golikipa wao Deo MUnish kuwa makini langoni. Mpka mwisho wa mchezo Azm 0 0 Yanga na kuifanya yanga ijiongezee alama moja halikazalika hivyohvyo kwa Azam.
Mchezo mwingine ni kule Mabatini ambapo wenyeji Ruvu Shooting waliilaza Mbeya city kwa goli moja.

Mtibwa wamekwenda Sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons, wakati huko ccm kirumba Vijana wa Kali Ongala Majimaji ya Songea waliilaza Toto Afrikan ya Mwanza kwa magoli mawili  kwa moja.



0 comments:

Post a Comment