Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kwamba Kiungo wao wa kimataifa wa Rwanda Mbuyu Twite ameongeza mkataba katika klabu hiyo.
Ikiwa tayari Yanga imefanikiwa kuwasajili wachezaji wawili golikipa Beno Kakolanya kutoka Tanzania Prisons na beki wa pembeni Vicent Andrew kutoka Mtibwa Sugar, wametangaza kumuongezea mkataba kiungo wao wa kimataifa wa Rwanda Mbuyu Twite.
Yanga wamemuongezea mkataba wa miaka miwili Mbuyu Twite hivyo ataendelea kuitumikia klabu hiyo kwa misimu mingine miwili.
Wakati Twite mambo yakimwendea sawa, kiungo wa kimataifa wa Niger Issafou Boubacar,amepewa barua ya kuvunja mkataba na sasa atakuwa huru kujiunga na timu nyingine itakayomuhitaji.
0 comments:
Post a Comment