Sunday, June 19, 2016

SIMBA YANASA KIFAA KINGINE KIPYA

Klabu ya Simba imempa mkataba wa miaka miwili kiungo Mohamed Ibrahimu tayari kwa kuitumikia klabu hiyo msimu ujao.

Rais wa Simba ameyathibitisha hayo kwa kusema usajili wa Ibrahimu utasaidia kuimarisha timu yao ambayo ina ukame wa mataji kwa miaka mitatu mfululizo.

"Ni kweli tumempa mkataba wa miaka miwili jana mchana, na bado tunaendelea kufanya mazungumzo na wachezaji wengine, lengo letu ni kujenga timu yetu na kpia kuhakikisha msimu ujao tunafanya vizuri." alisema Aveva.

"tulikuwa hatutaki kuona masuala yetu ya usajili yanafanyika kwa uwazi kwa sababu nusu ya wachezaji tunaowahitaji kwa ajili ya kuwasajili wana mikataba na timu zao, hivyo inabidi tumalizane kwanza na klabu zao ndio tunaweka wazi" aliongeza Rais huyo.

Meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo amekiri taarifa hizo kuwa Ibrahimu "Rasta" amesaini mkataba wa miaka miwili na Simba.

"Rasta amesaini mkataba jana, na hapa ninapoongea ndiyo tunamalizana kwa maana ya kusaini mkataba huo wa miaka miwili." alisema Kisongo.

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa

Related Posts:

  • "SINA MPANGO WA KUHAMIA SIMBA" JEBAKiungo Ibrahimu Jeba wa klabu ya Mtibwa Sugara amesema hana mpango wa kuihama Mtibwa Sugar kwa sasa. Simba walionyesha nia ya kumuhitaji kiungo huyo lakini yeye mwenyewe amedai hana mpango wa kuhamia klabu hiyo, Jeba amese… Read More
  • UKIMYA WA VIONGOZI WAMFANYA BEKI ASAKE KLABU SIMBAMiraji Adam ni mchezaji wa Simba ambaye alikuwa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Coastal Union ambayo kwa sasa imeshuka daraja huku yeye akisema yupo tayari kucheza katika klabu yoyote. Mkataba wa Miraji na Simba unaelek… Read More
  • HUYU NDO ANAYETARAJIWA KUWA KOCHA MPYA SIMBABaada ya kumkosa Kalisto Pasuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zimbabwe Simba walielekeza macho yao kwa kocha raia wa Ghana Sellas Tetteh Teivi Simba wanakaribia kumpata kocha huyo baada ya mazungumzo kwenda vizuri, Sellas… Read More
  • KIUNGO MPYA SIMBA TISHIO KWA MKUDE, NDEMLASimba imefanikiwa kumsajili Kiungo Mzamiru Yasini akitokea katika klabu ya Mtibwa Sugar. Yasini amesema hayupo tayari kukaa benchi hivyo atahakikisha anapambana na wakongwe ili kujihakikishia nafasi yake katika kikosi cha … Read More
  • CHIRWA ATUA JANGWANI KWA SH. MILIONI 240Mshambuliaji raia wa Zambia, Obrey Chirwa amejiunga na Yanga kwa dau la sh. Milioni 240 akitokea katika klabu ya FC Platinum za Zimbabwe. Chirwa ameifungia Platinum mabao matano katika mechi nane alizocheza kwenye ligi kuu… Read More

0 comments:

Post a Comment