Wednesday, June 8, 2016

BEKI WA BLACK LEOPARDS YA AFRIKA KUSINI KUTUA SIMBA

Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba Hans Poppe yupo katika mazungumzo na Beki wa kati wa klabu ya Black leopards ya nchini Afrika kusini Harry Nyirenda.


Hans Pope yupo nchini Zimbabwe kukamilisha usajili wa kocha Kalisto Pasuwa sambamba na kufanya mazungumzo na beki wa kati anayecheza katika klabu ya Black Leopards ya nchini Afrika kusini.

Harry Nyirenda raia wa Malawi ameonyesha kiwango kizuri kilichomvutia Hans Pope wakati timu yake ya taifa ya Malawi ilipocheza na Zimbabwe na hivyo kumuona kuwa ni mbadala mzuri wa Juuko Murshid aliyetimka katika kikosi cha Simba.



"Nimevutiwa na uwezo wake akiwa na timu ya taifa ya Malawi ilipocheza na Zimbabwe, nadhani anaweza kuwa msaada mkubwa kwetu kama tutafanikiwa kumpata ili kusaidiana na Novaty Lufungo" alisema Hans Pope alipozungumza na Goal.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo tayari wameshaanza mazungumzo na beki huyo na kama mambo yataenda sawa basi moja kwa moja mashabiki wa Simba watashuhudia beki huyo akitua katika klabu yao.

Related Posts:

  • MATOKEO UCHAGUZI YANGAMATOKEO YA UCHAGUZI MKUU WA YANGA ULIOFANYIKA JANA. M/KITI 1. Yussuf Mehboob Manji MAKAMU M/ KITI 1. Clement Sanga Wajumbe 8 Yanga ni:- 1. Omary Ameir 2. Siza Lyimo 3. Salum Mkemi 4. Thobius Lingalangala 5. Ayoub Nye… Read More
  • SERENGETI BOYS YAINGIA MZIGONITimu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeingia kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana. Serengeti Boys iliingia kambini jana chini ya koch… Read More
  • HUKU NDIKO SIMBA WANAKOSAKA NYOTA WAPYA Klabu ya Simba ipo katika pilikapilika za kuhakikisha wanaimarisha kikosi chao lengo likiwa ni kutwaa ubingwa wa ligi msimu ujao. Katika kuhakikisha wanafanya usajili wa uhakika Simba imeelekeza nguvu zake nchini Uganda,… Read More
  • USAJILI YANGA NI MWENDO MDUNDOKlabu ya Yanga imesema bado ina mipango ya kusajili wachezaji wa kimataifa kwa ajili ya kukisaidia kikosi chao kufanya vizuri katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika (CAF CC). Yanga imeshawanasa wachezaji wann… Read More
  • KIFAA KIPYA CHAAHIDI MAKUBWA SIMBAKiungo mshambuliaji aliyesajiliwa na Simba hivi karibuni Jamali Mnyate amesema kusaini kwake Simba mkataba wa miaka 2 ni kujiendeleza kimpira na kuisaidia Simba kupata mataji. Mnyate aliyejiunga na Simba akitokea Mwadui F… Read More

0 comments:

Post a Comment