Saturday, June 3, 2017

Tetesi Mpya Za Usajili Liverpool

Klabu ya Liverpool imefuzu kushiriki michuano ya klabu Bingwa Barani Ulaya UEFA Champions League msimu ujao wa 2017/18. Kuelekea katika michuano hiyo na ligi kuu nchini England, klabu hiyo imeshaanza kuziwania saini za wachezaji mbalimbali kama ambavyo Soka24 inakuletea kiundani yote yanayoendelea katika klabu hiyo.


Roma wakataa Ofa ya Liverpool
Majogoo wa London Liverpool, waliweka mezani kitita cha paundi milioni 28 kuitaka saini ya Winga Mohamed Salah lakini ofa hiyo imekataliwa, kwa mujibu wa Daily Mail.
Wababe hao wa Seria A wanadai gharama ya kuipata saini ya Salah ni paundi milioni 40.


Vita ya kumuwania Mendy Yapamba Moto.
Liverpool imeingia katika vita ya kutaka kuinasa saini ya beki wa Monaco Benjamin Mendy anayewaniwa pia na vilabu vya Chelsea na Manchester City. Beki huyo ameonyesha wazi kuwa anataka kucheza ligi kuu ya Uingereza msimu ujao, hata hivyo Barcelona nao wameonesha nia ya kumtaka beki huyo. Kwa mujibu wa L'Equipe

Gotze Kuchukua Nafasi ya Coutinho Liverpool
Kukiwa kuna sintofahamu juu ya kiungo wa Liverpool Phillippe Coutinho kama atabaki klabuni hapo kwa msimu ujao au atatimkia Hispania ambako anatakiwa na klabu ya Barcelona, Liverpool imeanza mbio za kumfukuzia Mario Gotze ili aje kuwa mbadala wa Coutinho endapo ataondoka klabuni hapo.

Casillas Kutua Liverpool?
Mlinda mlango wa zamani wa klabu ya Real Madrid Iker Casillas huenda akajiunga na majogoo wa jiji la London katika kipindi hiki cha usajili, kwa mujibu wa AS.
Taarifa zinadai kuwa mkongwe huyo tayari alifanya makubaliano ya awali na Liverpool ambao wanarudi kushiriki Champions League msimu ujao.

Liverpool yaongoza mbio za kumuwania Chamberlain.
klabu ya Liverpool inaongoza katika mbio za kuiwania saini ya kiungo Alex Oxlade-Chamberlain kwa mujibu wa The Sun.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza anatafuta changamoto mpya sehemu nyingine baada ya kuwa ameitumikia klabu yake ya Arsenal kwa miaka sita hivi sasa.

Tiemoue Bakayoko katika mipango ya Liverpool
klabu za Manchester United na Liverpool wanapigana vikumbo kuhitaji saini ya nyota wa Monaco Tiemoue Bakayoko, kwa mujibu wa Daily Mail.
Gazeti hilo limeripoti kuwa klabu hizo zitachuana pia na Chelsea ambao nao wanamuhitaji mchezaji huyo.

Gray Akaribia Kutua Anfield
klabu ya Liverpool kuwapiku Everton na Tottenham katika kuifukuzia saini ya Demarai Gray mshambuliaji wa Leicester City, kwa mujibu wa Mirror.

Madrid Yamtaka Wijnaldum
klabu ya Real Madrid inahitaji kumsainisha Gini Wijnaldum kutokana na uwezekano wa kumpata Eden Hazard kuendelea kuwa mdogo, kwa mujibu wa Tuttomercatoweb.
Wababe hao wa La Liga tayari wameshakaa na wakala wa kiungo huyo wa Liverpool ili kuhakikisha dili hilo linatimia.

Barcelona yatenga paundi milioni 51 kuinasa saini ya Coutinho.
Barcelona wamedhamiria kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil katika kipindi hiki cha usajili, kwa Mujibu wa Sport

Fabregas Kutua Liverpool
Liverpool ipo katika mipango ya kumnasa Fabregas kwa mujibu wa Daily Star.

Sessegnon Kuchukua Mikoba ya Moreno Liverpool
Livepool inajitahidi kukamilisha dili la kumsaini Ryan Sessegnon wakati ambao Alberto Moreno akiwa mbioni kuondoka klabuni hapo. Kwa mujibu wa Liverpool Echo.

0 comments:

Post a Comment