Friday, December 16, 2016

MASHARTI LIGI KUU VODACOM DURU LA PILI

Duru la Pili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuanza kesho Jumamosi Desemba 17 kwa michezo minne kabla ya michezo mingine minne kufanyika siku ya Jumapili Desemba 18, mwaka huu.

Katika mechi za kesho, Mabingwa watetezi wa taji hilo, Young Africans SC ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Licha ya kwamba mwenyeji wa mchezo huo ni JKT Ruvu ambayo uwanja wake wa nyumbani mara nyingi huwa ni Mabatini ulioko Mlandizi, lakini kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (5) na (6) ya Ligi Kuu Bara, mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba, Young Africans na Azam FC, hufanyika Uwanja wa Uhuru.

Michezo mingine ya kesho ni Kagera Sugar kuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Ruvu Shooting ya Pwani itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani ilihali Mwadui ya Shinyanga itaikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Mwadui Complex.

Jumapili, Desemba 18, mwaka huu Mbao FC ya Mwanza itacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati Ndanda itakuwa mwenyeji wa Vinara wa Msimamo katika Ligi Kuu ya Vodacom, Simba kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

African Lyon ya Dar es Salaam itaikaribisha Azam FC pia ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru jijijini siku hiyo ya Jumapili wakati Majimaji ya Songea itakuwa Mbeya kucheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, limetoa masharti kadhaa likitaka klabu za Ligi Kuu ya Vodacom kufuata.

Masharti hayo, ni kwa klabu kutumia makocha wenye sifa kwa mujibu wa kanuni ya 72 ya Ligi Kuu ya Vodacom. Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) na kwa mujibu wa kanuni hiyo, makocha wanaopaswa kukaa kwenye benchi la Ligi kuu kwa msimu huu wasipungue sifa ya kuwa na leseni B ya CAF.

Pia kwa timu za Ligi Daraja la Kwanza na Pili, masharti ni lazima makocha wawe na sifa za kuzinoa timu hizo ambazo zimeanishwa kwenye kanuni za ligi husika.

Kadhalika, tunaagiza klabu kutotumia wachezaji wa kigeni au makocha kama hawana vibali vya ukaazi na kufanya kazi kutoka Idara ya Uhamiaji nchini iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
CHANZO: TFF

Related Posts:

  • Yaliyosemwa Na TFF Kuhusu Yanga Na Azam Haya Hapa Rais Wa TFF Jamali Malinzi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri klabu za Azam FC na Young Africans ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa itayochezwa wikiendi hii. TFF i… Read More
  • Hizi Ndio Mbinu Zitakazowaua Al Ahly Taifa Kocha Mkuu wa Yanga YANGA inajiandaa kufungasha virago vyao kutoka Kisiwani Pemba ilipoenda kujichimbia kwa siku chache kujiandaa na mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini ikiwa huko Vijana wa Jangwani wamepewa mbin… Read More
  • Yanga Yatakiwa Kufanya Uchaguzi Wiki Ijayo Waziri wa Michezo Mh. Nape Kushoto Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imeandikia barua klabu ya Yanga kuiagiza iwe imekwishafanya uchaguzi wake hadi kufika Aprili 15, mwaka huu. Yanga imekwishapokea barua hiyo ku… Read More
  • Joseph Kimwaga Ajutia Kutua Msimbazi kimwaga Kushoto akishangilia goli Sraika wa Simba, Joseph Kimwaga ametamka kuwa kati ya vitu ambavyo anajutia kwenye maisha yake ya soka, basi ni kutua kuichezea timu hiyo.Mshambuliaji huyo alitua kuichezea Simba kwen… Read More
  • Wadhamini Wa UEFA Kuboresha Soka La Tanzania Shirikishio la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeishukuru kampuni ya bia ya Heineken ambao ni wadhamini wakuu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (UEFA) kwa kujitolea kufanya ukarabati wa viwanja vitatu vya mpira w… Read More

0 comments:

Post a Comment