Kessy amesajiliwa na Yanga akitokea Simba na amezuiwa kucheza kutokana na mkataba wake na Simba kuwa unamalizika Juni 30 kitu kilichomfanya pia akose mechi ya kwanza Yanga dhidi ya MO Bejaia.
Licha ya kupokea usajili wa Kessy CAF, inahitaji barua kutoka kwa Simba ya kumwidhinisha beki huyo kuichezea Yanga kwenye michuano hiyo.
Muro alisema kuwa klabu ya Yanga imewaandikia barua Simba kutaka ruhusa ya Kessy na kwamba nakala ya barua hiyo waliiwasilisha TFF ili kama Simba watachelewa kujibu barua hiyo TFF wachukue hatua.
Lakini kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba kupitia mkuu wa kitengo cha habari Haji manara ni kwamba wao kama Simba hawajapokea barua yoyote kutoka kwa Yanga.
"Hakuna barua yoyote ambayo Yanga imetuandikia kuhusiana na Kessy, pia hakuna mazungumzo yaliyofanyika baina ya viongozi wa klabu hiyo ili kutuomba walau kwa mdomo kama taratibu zinavyotaka, ikumbukwe Simba haina tatizo kuhusu matakwa binafsi ya mchezaji na nyote mnajua utamaduni wa klabu yetu" alisema Manara.
Msemaji huo aliongeza kuwa pamoja na maneno ya kuudhi kutoka kwa Yanga, wao Simba ni waungwana na wao wasitumie ukimya wao kuwapotosha wanachama na mashabiki, kwa kusema wamekataliwa kuwajibu barua ya Kessy.
0 comments:
Post a Comment