Thursday, April 7, 2016

MATOKEO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE


UEFA Champions league iliendelea tena jana kwa mechi mbili zikizikutanisha timu za PSG VS MAN CITY na WOLFSBURG VS REAL MADRID ambapo mechi kati ya PSG dhidi ya MAN CITY iliisha kwa sare ya kufungana 2 - 2, MAN CITY iliandika goli la kwanza kupitia kwa Mshambuliaji wake De Bryune  mnamo dakika ya 37', lakini goli hilo halikudumu sana baada ya Zlatan Ibrahimovic kusawazisha dakika ya 41'.
hadi timu zinakwenda mapumziko PSG 1 - 1 MAN CITY, kipindi cha pili kilianza kwa kasi hali iliyopelekea PSG kuandika goli la pili dakika ya 59' kupitia kwa A.Rabiot, lakini Man City hawakurudi nyuma wakaelendelea kucheza kwa kujituma na mnamo dakika ya 72' Mshambuliaji Fernandinho alifanikiwa kuisawazishia Man City, hadi mechi inaisha PSG 2 - 2 MAN CITY.
upande wa pili wababe wa La Liga Real Madrid wamepokea kichapo cha paka mwizi baada ya kugaragarazwa bila huruma na Wolfsburg kwa jumla ya magoli 2 - 0 huku Christiano Ronaldo akishindwa kuwika katika Mechi hiyo. Magoli ya Wolfsburg yalifungwa na R.Rodriguez dakika ya 18' na M.Arnold dakika ya 25'.
Matokeo haya yanaziweka pazuri timu za Man City na Wolfsburg katika mbio za kuwania kikombe cha UEFA Champions league 2015/2016.

Related Posts:

  • HATIMA YA VAN GAAL MAN UNITED YAWEKWA WAZI Louis Van Gaal amehakikishiwa na mabosi wa United kuwa ataendelea kubaki katika klabu hiyo hadi mwisho wa mkataba wake kwa mujibu wa ripoti ya Daily Star. Mdachi huyo anayeinoa United amekuwa akisemwa sana juu ya uwezo … Read More
  • SUPER MARIO AKUBALI KUJIUNGA NA MAN UNITED Manchester United wanakaribia kumalizana na mchezaji wa Sporting Lisbon Joan Mario. Mabosi wa United wamefanya mazungumzo mara kadhaa na mchezaji huyo mwenye miaka 23 raia wa Ureno na wakala wake anaamini dili hilo li… Read More
  • KLABU 5 TAJIRI ZAIDI DUNIANI 2016 Real Madrid imetajwa kuwa ndio klabu tajiri zaidi duniani kwa mara ya 4 mfululizo, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Forbes. Wababe hao wa Hispania Walibeba taji la Uefa Super Cup na Klabu Bingwa duniani (Fifa Club W… Read More
  • BARCELONA WATETEA UBINGWA WAO Barcelona imetwaa ubingwa wa La Liga baada ya kuifunga Granada kwa jumla ya magoli 3 – 0 magoli yote yakifungwa na Luis Suarez, Barcelona wametwaa ubingwa huo kwa tofauti ya pointi 1 tu na mahasimu wao wakubwa Real Madri… Read More
  • LEWANDOWSKI AIFIKIA REKODI ILIYOWEKWA MIAKA 39 ILIYOPITA MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Borrusia Dortmund anayekipiga katika klabu ya Bayern Munich kwa sasa Robert Lewandowski amefikia rekodi iliyowekwa miaka 39 iliyopita katika ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundeslig… Read More

0 comments:

Post a Comment