Wednesday, June 8, 2016

KINACHOCHELEWESHA DILI LA IBRAHIMOVIC MAN U HIKI HAPA

Klabu ya Man United itasubiri kumsajili Zlatan Ibrahimovic hadi Juni 30, mwaka huu.


Manchester United itamruhusu Zlatan Ibrahimovic kusubiri hadi mkataba wake ambao umebakiza mwezi mmoja katika klabu yake ya PSG umalizike ndipo wao wamsajili.
Hivyo mashabiki wa United wanalazimika kusubiri hadi tarehe hiyo ndipo wamkaribishe rasmi Supastaa huyo katika dimba lao la Old Trafford.

Zlatan na wakala wake watapata kiasi cha Paundi milioni 4 kama bonasi Kutoka kwa PSG pale mkataba wa Ibrahimovic utakapomalizika kabisa.

Ibrahimovic 34, anatarajiwa kuungana na kocha wake wa Zamani ambaye alimfundisha soka wakati huo Zlatan akiwa Inter Milan na Mourinho akiwa Meneja wa timu hiyo.

Ed Woodward, makamu mwenyekiti wa klabu ya United alitamani saini ya Ibrahimovic kabla ya michuano ya kombe la ulaya (Euro 2016) haijaanza lakini atalazimika kusubiri hadi mkataba wa Ibrahimovic umalizike kabisa.

0 comments:

Post a Comment