Arsenal wanahitaji kuboresh kikosi chao katika eneo lao la
ushambuliaji, ambalo linaonekana kutokuwa imara kulikochangiwa pia na kuondoka
kwa Mshambuliaji Robin Van Persie aliekajiunga na mahasimu wao Man United.
Ufungaji wa magoli katika kikosi hicho umekuwa si wa uhakika
sana, safu hiyo ikiongozwa na Olivier Giroud na Danny Welbeck wanaofanya vizuri
lakini si kwa kiwango kile cha Mholanzi Van Persie.
Kupata magoli hasa katika mechi za nyumbani limekuwa ni
tatizo ambalo Arsenal wanapaswa kulifanyia kazi na bila shaka wanalijua hilo na
watalifanyia kazi katika msimu ujao wa usajili.
Hapa nimekuwekea wachezaji watatu wanaocheza ligi kuu ya
Italia Seria A ambao endapo watatua Arsenal basi watakuwa wameimarisha safu yao ya
ushambuliaji.
3. MAURO ICARD (INTER MILAN)
Huyu ni Muagentina mwenye miaka 23 ambae ubora wake katika
eneo la ushambuliaji limemfanya atambulike katika ulimwengu wa soka duniani.
Icard ni mchezaji wa zamani wa Barcelona katika kikosi cha vijana, alianza
kwa kujiunga na Sampdoria na badae kujiunga na Inter amekuwa na mchango mkubwa
sana klabuni hapo. Kwa sasa ni nahodha wa Inter Milan na anauwezo mkubwa
unaomfanya awe forward mzuri kitu ambacho Arsenal wanakikosa kwa sasa.
Katika misimu mitatu amefunga jumla ya magoli 51 akiwa Inter
katika mashindano yote na kiwango chake bado kinaonekana kukua zaidi, haitakuwa
rahisi kumtoa Inter lakini kutua kwake Arsenal utakuwa ni uwekezaji mkubwa sana
kwa klabu.
Ni mzuri katika umaliziaji na anaujuzi wa kumiliki mpira, na
huwa anajua kuzitumia chance anazozipata katika kuwashangaza mabeki wa timu
pinzani.
Mauro Icard |
2. ALVARO MORATA (JUVENTUS)
Morata ni straika wa tofauti ukimlinganisha na Icard,
mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid ni Straika mzuri sana katika kuunganisha
timu, ni mchezaji ambae anauwezo wa kuwaweka wachezaji wenzake katika mchezo,
na atakuwa na mchango mzuri sana Arsenal.
Giroud anafanana kiuchezaji na Morata lakini uwezo wa
umaliziaji wa Morata ni mkubwa zaidi ukilinganisha na Giroud na utakuwa ni
muunganiko mzuri sana akitua Arsenal akishirikiana na Mesut Ozil na Alex
Sanchez.
Kwa sasa hana uhakika sana wa kuanza katika kikosi cha
kwanza na hiyo inaweza kumfanya awe sokoni katika msimu ujao wa usajili.
Alvaro Morata |
1.. GONZALO HIGUAIN (NAPOLI)
Higuan ni mchezaji mzuri aliyekatika level za juu katika
rekodi za soka duniani, amefunga magoli 30 katika mechi 32 alizocheza msimu huu
katika ligi ya Itali Seria A na endapo Arsenal wakiliona hilo na kumsajili atakuwa
na mchango mkubwa sana katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo. Higuan huwa
anatumia vizuri makosa ya mabeki wa wapinzani. Arsenal hawajawahi kuwa na
straika wa kaliba ya Higuan kwa misimu ya hivi karibuni. Mchezaji ambaye
amekamilika katika kila idara na endapo Mzee wenga ataamua kumwongeza katika
kikosi chake ni wazi kuwa atakuwa ni chanzo cha magoli katika klabu ya Arsenal.
Gonzalo Higuan |
Je, Unadhani moja kati ya Wachezaji hawa atasaidia kutatua
matatizo ya safu ya Ushambuliaji Arsenal? Weka COMMENT yako katika sehemu ya
comment hapo chini.
0 comments:
Post a Comment