Friday, April 29, 2016

SIMBA WAREJEA DAR TAYARI KWA KUIVAA AZAM FC


TIMU ya Simba Sports Club imewasili jijini Dar wakitokea visiwani Zanzibar ambako walikwenda kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Azam FC. Simba inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kujiweka katika nafasi mzuri zaidi ya kushindania taji hilo la ligi msimu huu. Siku za hivi karibuni kumekuwa na kutokuelewana kwa baadhi ya wachezaji wa Klabu hiyo na kocha Mayanja kwa kile kinachoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu wa wachezaji hao. Simba inahitaji kutulia na kuweka tofauti zao pembeni kwa kipindi hiki ambacho ligi inaelekea ukingoni ili kuleta hamasa klabuni hapo na hatimaye kuchukua ubingwa wa ligi kuu. Mashabiki ambao walionekana kukerwa sana na matokea dhidi ya Coastal ambapo Simba walifungwa goli moja kwa bila wanatakiwa kuwa na subra na uvumilivu katika kipindi hiki na kuipa support timu yao ili ifanye vizuri.
Kwa upande mungine Kiungo mkabaji wa kimataifa wa klabu hiyo Justice Majabvi ambae alikuwa majeruhi nae alishiriki mazoezi ya timu wakiwa huko visiwani Zanzibar chini ya uangalizi wa Daktari wa timu Yassin Gembe na huenda kocha Mayanja akamtumia katika mechi yao dhidi ya Azam FC itakayochezwa siku ya Jumapili hii.

Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment