KLABU ya Dar Young Africans imeendelea na mazoezi huko mwanza katika viwanja vya DIT wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya Toto Africans ambao utachezwa siku ya Jumamosi April 30, Yanga ambayo inashika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi, wanaelekea katika mchezo huo huku wakijua wazi msimamo wa ligi bado hauwahakikishii ushindi wa moja kwa moja wa ligi ukizingatia wamebakiwa na mechi 5 ambazo zote watacheza ugenini na hivyo kuhitaji ushindi katika mchezo huo, na tumeshuhudia timu za Azam, Yanga na Simba zikikumbana na changamoto za viwanja hasa vya mikoani. Bado msimamo wa ligi uko wazi na unatoa nafasi kwa timu yoyote ambayo itazimalizia vizuri mechi zake zilizobaki kuchukua ubingwa wa ligi kwa msimu huu.
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment