Friday, June 3, 2016

SAKATA LA ULAGHAI WA KODI, MESSI ATOA USHAHIDI

Supastaa wa Soka Duniani raia wa Argentina, Lionel Messi ametoa ushahidi katika mahakama ya Uhispania kuhusu sakata lake la kukwepa kulipa kodi.

Lionel Messi



Nyota huyo wa Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina ametoa ushahidi kuhusu suala hilo katika mahakama ya nchini Hispania kutokana na tuhuma zinazomkabili za ukwepaji wa kodi anaotuhumiwa kuufanya akishirikiana na baba kati ya mwaka 2007 na 2009 zaidi ya Uro milioni 4.

Mamlaka ya Ushuru nchini Hispania inadai kuwa Messi na Baba yake walitumia kampuni zao zilizopo Belize na Uruguay kuficha mapato yao yanayotokana na haki za picha zao.

Staa huyo wa klabu ya Barcelona aliwasili mahakamani nchini Hispania jana Alhamisi kutoa ushahidi wa mashtaka hayo akiongozana na baba yake Jorge Horacio.

Messi katika utetezi wake alisema yeye hakuwa anajua chochote kinachoendelea kuhusu pesa zake kwani baba yake na wanasheria wake ndo walikuwa wanashughulikia masuala yake ya fedha wakati yeye akiendelea na majukumu yake Barcelona.
Messi na Baba yake Wakiwa Mahakamani

"Nilikuwa nacheza mpira. Sikuwa najua kitu chochote kinachoendelea" alisema nyota huyo mahakamani hapo
.
"Nilimuamini baba yangu na wanasheria wangu" aliongeza Messi.

"Ninachojua mimi ni kwamba tulisaini makubaliano na wadhamini kwa kiasi "X" cha pesa na nilitakiwa kufanya matangazo, picha  na vitu kama hivyo, lakini kuhusu pesa na wapi zilikwenda sijui kitu chochote" alisema Messi.

Mahakamini hapo palifurika waandishi wa habari, wapiga picha na watu mbalimbali walioenda kujua kinachoendelea katika kesi hiyo. Wapo waliomshangilia Messi huku wengine wakimtolea maneno makali.

"Kama amedanganya, anatakiwa afungwe jela bila kujali umaarufu wake na ushindi wake wa Ballon d'Or mara 5. Hizi ni Euro milioni 4 ambazo zingetumika mahospitalini, mashuleni, kwa zimamoto na hata kuboresha barabara" alisema Jose Seco de Herrero akimwambia mwandishi wa habari wa AFP.

"Mwizi!!" alisikika mtu mmoja akisema kwa sauti kubwa, "Nenda Kacheze Panama" alisema Mwingine.

Messi na baba yake hawatahudhuria mahakamani hapo mara ya mwisho ambapo wanasheria watatoa uamuzi wa kesi hiyo.
Hakuna tarehe iliyotajwa kwa mahakama hiyo kutoa uamuzi wake.

Endapo itabainika kuwa Messi na Baba yake walifanya kosa hilo, basi dunia itashuhudia Nyota huyo Mshindi mara 5 wa tuzo ya mchezaji bora duniani akihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.


Related Posts:

  • MASHABIKI 17 WA LIVERPOOL WATIWA NDANI Mashabiki 17 wa Liverpool walitiwa kizuizini na kuachiwa kufuatia matukio yaliyojitokea katika mchezo wa fainali Europa League Jana. Police wa Basel waliwakamata mashabiki 30 na kuwaweka ndani 17 wakiwa ni wa Liverpo… Read More
  • HOFU YA UGAIDI MICHUANO YA EURO 2016 YATANDA Ufaransa na Ujerumani zimetoa angalizo kwamba kikundi cha kigaidi cha ISIS kinapanga kufanya mashambulizi katika michuano ya Euro 2016 Katika mataifa yote yatakayoshiriki Euro 2016 Ufaransa pekee ndiyo inakuwa katika h… Read More
  • HUYU NDO ALIYEIFUNGISHA LIVERPOOL KWENYE FAINALI EUROPA Liverpool imepoteza mchezo wake wa fainali dhidi ya Sevilla kwa kufungwa magoli 3 - 1 na Alberto Moreno ndo ameonekana kuiangusha timu. Liverpool imepoteza katika mchezo wake wa fainali kombe la Europa jana baada ya ku… Read More
  • SERENGETI BOYS YATINGA NUSU FAINALI Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ leo Mei 19, 2016 imetinga hatua ya Nusu Fainali baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Korea Kusini  Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wen… Read More
  • SPURS NA ARSENAL KUWANIA SAINI YA MIDFIELD RAIA WA KENYA Tottenham Na Arsenal Wanasaka Saini Ya Midfieda Wa Southampton Victor Wanyama Wanyama alikuwa karibu kujiunga na Tottenham msimu uliopita lakini dili hilo lilifeli. Inasemekana Spurs bado wanania ya kumsajili Wanyama w… Read More

0 comments:

Post a Comment