Friday, June 3, 2016

TANZANIA YAPOROMOKA KATIKA UBORA WA VIWANGO VYA SOKA DUNIANI

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeshuka kwa nafasi 7 kutoka nafasi ya 129 hadi 136 katika ubora wa viwango vya soka duniani.


Algeria imeendelea kushika nafasi ya kwanza barani Afrika huku ikiwa imepanda katika viwango vya dunia kwa nafasi moja na kufikia nafasi ya 32, ikifuatiwa na Ivory Coast na Ghana ambazo ndo zinashika tatu bora barani Afrika.


Fifa imetoa viwango hivyo wakati Stars ikijiandaa kukabiliana na Misri katika mchezo wa kutafuta nafasi ya kufuzu kushiriki michuano ya mataifa huru barani Afrika.

0 comments:

Post a Comment