Timu ya taifa ya Uingereza imeendelea na maandalizi yake kujiandaa na michuano ya Euro 2016 itakayofanyika chini Ufaransa kuanzia Juni 10 mwaka huu, baada ya jana kuifunga Ureno katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Chris Smalling ndiye alipeleka ushindi kwa upande wa England baada ya kumalizia vizuri kwa kichwa mpira uliopigwa na Raheem Sterling aliyeingia akitokea benchi na kuandika goli hilo pekee la ushindi mnamo dakika ya 86 ya mchezo.
Hatahivyo Ureno walicheza wakiwa pungufu baada ya mlinzi wake wa kati Bruno Alves kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea faulo mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane dakika ya 35.
0 comments:
Post a Comment