Friday, June 3, 2016

KAMATI YA OLIMPIKI YA KIMATAIFA (IOC) YATOA ANGALIZO

Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa imetangaza hatua mpya zitakazotumika kuondoa udanganyifu wa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni katika michuano ya Olimpiki Mjini Rio de Janeiro.




Kamati hiyo imesema kuwa itaongeza bajeti ya Vipimo hasa kwa wanariadha kutoka nchi za Urusi, Kenya na Mexico, Hatua hiyo inakuja kufuatia nchi hizo tatu kuwa chini ya viwango vilivyowekwa na shirika la kupambana na dawa zilizopigwa marufuku michezoni.

Aidha kamati hiyo imeahidi kuendeleza upelelezi wake wa sampuli za awali katika mashindano yaliyofanyika Beijing na jijini London.

Wanariadha wanaokadiriwa kufika 50 wanatuhumiwa kutumia dawa hizo, 22 kati ya hao wakiwa ni raia wa Urusi.

0 comments:

Post a Comment