Sunday, June 5, 2016

MASHABIKI WA LEICESTER CITY WAMJIA JUU MKEWE VARDY NAE AWAJIBU

Habari kubwa za usajili kwa sasa barani ulaya ni pamoja na ile inayomuhusisha Jamie Vardy kujiunga Arsenal na taarifa hizo zimepokelewa vibaya na mashabiki wa Leicester  City.


Straika huyo wa Leicester anatarajiwa kujiunga na The Gunners licha ya klabu yake kufuzu kucheza Champions League msimu ujao baada ya kushinda Ligi kuu nchini England.
Hali hiyo imepokelewa vibaya na mashabiki wa Leicester walioamua kumshambulia mkewe Vardy, Rebekah Vardy kupitia katika mitandao ya kijamii wakiamini kuwa anahusika kwa namna fulani katika kumshawishi mumewe kuihama klabu yake.

Rebekah ameshindwa kuvumilia mashambulizi hayo kutoka kwa mashabiki wa Leicester nae akaamua kuwajibu kwa kusema, yeye hahusiki na chochote juu ya uhamisho huo huku akisisitiza kuwa haingilii maamuzi yanayohusisha kazi ya mumewe, na kwamba wanachokifanya mashabiki wa Leicester kwake sio kitu cha busara.




Vardy amekuwa na mchango mkubwa katika klabu ya Leicester City na hivyo mashabiki wanahofu kuondoka kwake klabuni hapo huenda kukaiyumbisha timu yao ambayo inatarajiwa kushiriki michuano ya Uefa Champions League msimu wa 2016/17

0 comments:

Post a Comment