Manchester United iliwakaribisha Leicester jana katika dimba
la Olf Trafford, mechi ambayo Leicester City walikuwa wanahitaji kushinda ili
wajitangazie ubingwa wa ligi kuu nchini humo. Lakini Man United chini ya kocha
Louis Van Gaal hawakukubali vijana hao wa Ranieri wautwae ubingwa katika dimba
hilo la Old Trafford kwa kutoa sare ya 1 – 1.
Kama ilivyokawaida kwa makocha kusalimiana tena baada ya
mechi, ilitokea pia kwa makocha hao ambapo Claudio Ranier kocha wa Leicester
City alimwambia Louis Van Gaal kuwa
anafanya kazi nzuri sana klabuni hapo licha ya watu kumsema vibaya, Van Gaal
nae alimtakia kila la kheri Ranieri kwa kumwambia avute subra tu ila ubingwa ni
wa kwao msimu huu.
Leicester City wanatakiwa kusubiri hadi mechi yao ijao ili
endapo wakishinda watangazwe mabingwa wapya wa ligi au endapo leo Tottenham
Hotspurs watafungwa na Chelsea basi Leicester watakuwa moja kwa moja mabingwa
wa EPL msimu wa 2015/2016.
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment