Wakitokea benchi Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba dakika ya 62,
waliisadia timu yao ya Manchester United kuitoa timu ya Blackburn Rovers kwa
idadi ya goli 2 – 1.
Pongezi zote ziende kwa Paul Pogba ambae ndie aliefanya kazi nzuri
kupitia upande wa kulia na kutoa pasi nzuri ambayo ilimaliziwa kwa ustadi
mkubwa na Ibra na kuifanya united kuibuka kifua mbele.
Blackburn Rovers ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za
United mnamo dakika ya 17 pale Daniel Graham alipo malizia mpira kutoka kwa Marvin Emnes.
Baada ya goli hilo United walianza kulisakama lango la Rovers bila
mafanikio.
Dakika ya 27 Henrik Mkhitaryan alifanya kazi kubwa na kumpa nafasi
Marcus Rashford kuisawazishia United.
Mpaka mapumziko Blackburn Rovers1 – 1 Manchester United.
Kipindi cha pili dakika ya 62 Jose Mourinho aliwatoa Jesse Lingard
na Anthony Martial na kuwaingiza Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba, mabadiliko
ambayo yaliinufaisha United.
Dakika 75 Zlatan
Ibrahimovic alifanya kile alichotumwa na benchi la ufundi la United baada ya
kuukwamisha wavuni mpira ulitengwa na Paul Pogba .
mchezo mwingine leo ilikuwa ni kati ya Fulham waliokubali kichapo cha goli 3 kwa
bila toka kwa Tottenham Hotspur, kwa magoli ya Harry Kane 16', 51', 73'.
Kwa Matokeo haya Manchester inaoungana na Middlesbrough, Tottenham, Millwall, Lincoln, Chelsea katika robo
fainali.
Ratiba ya Robo fainali itakuwa hivi:-
Tottenham vs Millwall
Chelsea vs Manchester United
Sutton /Arsenal vs Lincoln
0 comments:
Post a Comment