Timu ya Simba leo asubuhi imeendelea kufanya mazoezi katika
Uwanja wa Amaan, simba ipo Unguja tangu ijumaa kwa maandilizi ya mchezo
na mtani wake Yanga.
Simba imefikia katika Hoteli ya Mtoni Marine iliyopo Maruhubi
Mkoa Mjini Magharibi, na tangu ijumaa mpaka jana ilikuwa inafanya
mazoezi yake asubuhi saa 3:00 – 5:00 katika dimba la Amaan.
Mratibu wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’ alipohojiwa na
baadhi ya waandishi wa habari wa hapa Zanzibar alisema kuhusu kufanya mazoezi
asubuhi tu alisema “wanafuata Ratiba ya mwalimu na kuanzia jumatatu watakuwa
wanajifua mara mbili asbubuhi na jioni katika dimba hilo”.
“simba watarejea Dar es saalam siku ya ijumaa wakiwa tayari
kwa mchezo wa jumamosi” aliongeza Mratibu huyo.
0 comments:
Post a Comment