Azam yapangwa na Mbabane Swallows
Mabingwa wa Afrika Mashariki na kati timu ya Azam
imepangwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa kombe la shirikisho na Mbabane Swallows
ya Swaziland.
Mbabane wameitoa timu ya Orapa
United ya Botswana kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya 1 – 1 katika Matokeo
ya jumla (aggregate).
Azam wao walikaa kusubiri mshindi
kati ya timu hizo mbili baada ya kufuzu baadhi ya vigezo vya CAF hivyo
kutoshiriki hatua ya awali.
Mshindi kati ya Azam na Mbabane
atajumuishwa na timu zitakazotolewa toka
ligi ya mabingwa, na kucheza hatua ya mwisho ya mtoano(playoff).
Katika michezo hiyo ya ‘playoff’
watapatikana washindi 16 ambao watapangwa katika makundi manne ya timu nne nne.
Azam wataanza kibarua cha kutimiza
ndoto zao za kufika kwenye makundi march 12 nyumbani Chamanzi, na kurudiana
wiki moja badae yani march 17, 18 au 19 huko Swaziland.
0 comments:
Post a Comment