Magoli miwili
ndani ya dakika 4 yameifanya Valencia kuibuka na ushindi mbele ya vinara wa
ligi kuu ya Hispania maarufu kama ’Laliga Santander’ Real Madrid .
Munir El
Haddadi alipokea mpira uliokolewa na na beki wa kati wa Valencia Ezequiel Garay
baada ya shambulizi kali langoni mwa Valencia. Munir El Haddadi alipiga jaro
zuri na kumkuta mfungaji Simone Zaza ambae bila ajizi aliweka mpira huo wavuni.
Real Madrid
wakiwa wanajiuliza wafanye nini ili warudishe goli dakika ya 9 Fabian Orellana
aliipatia Valencia goli la pili kufuatia kazi nzuri ya Nani.
Madrid
walionekana kupaniki baada ya goli hilo na kumshudia mchezaji bora dunia akiwa
anaongea kwa hasira dhidi ya wachezaji wenzake.
Badae Madrid
walirejea mchezoni na walifanikiwa kuutawala mchezo huo kwa kiwango kikubwa
ndani ya kipindi cha kwanza.
Dakika ya 44
Cristiano Ronaldo aliipatia Madrid goli baada ya kazi nzuri ya beki mbrazili
Marcelo.
Mpaka kipindi
cha kwanza kinamalizika Valencia 2 – 1 Real Madrid.
Kipindi cha
pili Real Madridi walirudi na nguvu ya kutafuta magoli zaidi lakini uimara wa
kulinda lango umeiwezesha timu ya Valencia kuibuka na ushindi huo.
Madrid walifanya
mabadiliko kadhaa kwa lengo la kuongeza nguvu kikosi chao kwa kuwaingiza Gareth
Bale 62’, Nacho Fernandez 73’ na Lucas Vazquez76’ kuchukua nafasi za James
Rodriguez 62’, Raphael Varane 73’ na Luka Modric 76’
Wakati Valencia
wao walifanya mabadiliko kwa lengo la kuhakikisha wanaiadhibu Madrid kwa
kuwaingiza Guilherme Siqueira na kutoa Nani 39’, Carlos Soler kuchukua nafasi
ya Fabian Orellana 54’ na walimtoa Simone
Zaza na kumuingiza Mario Suarez 74’.
Mabadiliko hayo
yaliiwezesha Valencia kuondoka na alama
zote tatu katika dimba la Estadio Mestalla mbele ya watazamaji 45833 na
kujikusanyia jumla pointi 26 baada ya michezo 23 katika nafasi ya 14.
Madrid wao
wamebaki kileleni wakiwa na pointi 52 baaada ya michezo 22 wakifuatiwa kwa
karibu na Barcelona wenye pointi 51 baada ya michezo 23.
Vikosi
Real Madrid:
Keylor Navas, Daniel Carvajal, Raphael
Varane, Sergio Ramos, Marcelo, Luka Modric, Toni Kroos, James Rodriguez, Karim
Benzema, Cristiano Ronaldo Casemiro.
Kocha: Zinedine Zidane
Mfumo: 4:3:3
Valencia: Diego Alves, Joao Cancelo ,Ezequiel Garay,
Eliaquim Mangala, Jose Gaya, Daniel Parejo, Enzo Perez, Munir El Haddadi, Fabian
Orellana, Nani, Simone Zaza
Kocha: Voro
Mfumo: 4:2:3:1
0 comments:
Post a Comment