Golikipa wa
timu ya Kagera sugar ya mkoani Kagera Juma Kaseja ametwaa tuzo ya mchezaji bora
ya mwezi January ambayo hutolewa kila mwezi na wadhamini wa ligi hiyo kampuni
ya Vodacom Tanzania.
Katika kinyang’anyiro
hicho Kaseja aliwashinda Jamal S. Mtengeta wa Toto Africans ya Mwanza na Mbaraka
Abeid wa Kagera Sugar.
Kaseja
atakabidhiwa kitita cha shilingi milioni moja ya kitanzania na wadhamini
Vodacom.
Katika mwezi
January Kagera imecheza michezo mitatu na kushinda yote na kuweza kutoka nafasi
ya tano hadi ya 3.
Katika michezo
yote mitatu kaseja alisimama langoni na kuruhusu goli moja pekee huku Kagera wakifunga
jumla ya goli 6.
0 comments:
Post a Comment