Monday, May 2, 2016

MAN CITY NA LIVERPOOL ZAPOKEA VICHAPO VIZITO


Ligi kuu Nchini Uingereza imeendela tena jana katika viwanja mbalimbali, katika mechi za awali Swansea iliwakaribisha majogoo wa London Liverpool Na mchezo mungine ulikuwa  ni Kati ya Southermpton na Manchester City.
Katika mechi ya Liverpool Jürgen Klopp alishuhudia vijana wake wakishushiwa kipigo kikali cha magoli 3 - 1 mchezo uliopigwa katika dimba la Liberty Stadium.Magoli ya Swansea yalifungwa Na Andre Ayew dakika ya 20 Na 67 Na lingine likifungwa Na J.Cork dakika ya 33, huku goli la kufutia machozi la Liverpool likifungwa Na Benteke dakika ya 65.
Vijana wa Manuel Pelegrin nao walishindwa kutamba mbele ya Southermpton baada ya kukubali kipigo cha magoli 4-2. Magoli ya Southermpton yamefungwa Na Mane aliepiga hat-trick akifunga dakika ya 28', 57' Na 68', lingine likifungwa Na Long dakika ya 20, wakati magoli ya Man City yakifungwa Na lheanacho dakika ya 44 na 78.
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment