Monday, May 2, 2016

VILLARREAL YAFUZU KUSHIRIKI UEFA CHAMPIONS LEAGUE MSIMU UJAO


KLABU ya Villarreal ya nchini Hispania imefuzu kushiriki mashindano ya Uefa Champions League msimu ujao baada ya ushindi wao wa jana dhidi ya Valencia. kama ilivyo katika ligi kuu ya nchini England, EPL kutoa timu 4 zinazoshiriki mashindano ya UCL na ndo hivyo hivyo pia katika ligi kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga. Timu 4 za juu, kwa maana ya zile zinazoshika nafasi ya 1,2,3 na 4 katika msimamo wa ligi hiyo ndio zinashiriki katika mashindano ya UEFA.

Villarreal wamingia top 4 baada ya kuishushia kichapo cha magoli 2-0 timu ya Valencia na kuwafanya kufikisha pointi 64 huku wakiwa wanashika nafasi hiyo ya 4 katika msimamo wa ligi hiyo. wanahitaji kumalizia vizuri mechi zao zilizobaki ili kujihakikishia zaidi ushiriki wao Uefa msimu ujao.
Tayari Barcelona, Atletico Madrid na Real Madrid walishafikia hatua hiyo kwa kujikusanyia pointi 85,85 na 84 kila mmoja.
Magoli ya Villarreal yamefungwa na Samu katika dakika ya 14' na Adrian 33'.

Alhamisi ya wiki hii Villarreal watacheza mchezo wao wa pili wa nusu fainali ya Europa League dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield, baada ya kushinda kwa goli 1 - 0 katika mchezo wa kwanza.

Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment