Monday, April 25, 2016

Gareth Bale Asisitiza Hana Bifu Na Christiano Ronaldo


Gareth Bale amekanusha uvumi unaomhusisha yeye kutokuwa na mahusiano mazuri na mchezaji mwenzie Christiano Ronaldo maarufu kama CR7, akisema ana mahusiano mazuri tu na mchezaji huyo na kamwe hajawahi kuingia katika mzozo na Ronaldo.

Wawili hao wanaunda timu hatari sana ya ushambuliaji Santiago Bernabeu, Bale alivunja rekodi ya dunia ya usajili iliyowekwa na Ronaldo wakati akihama kutoka Tottenhama kwenda Madrid mwaka 2013, lakini Muwelshi huyo (Bale) amesisitiza hana tatizo na Ronaldo.

Bale na Ronalo wanatarajiwa kufanya makubwa katika mchezo wao na Manchester City katika hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya UEAFA Champions League jumanne hii.

Akihojiwa kwenye interview Bale alisema “Yeye (Ronaldo) anazungumza kiingereza, kitu ambacho kilinisaidi sana nilipofika hapa (Madrid). Sisi pia (Bale na Ronaldo) wote tumetokea katika ligi moja ya Uingereza” .
“hatujawahi kuwa na tatizo, sijawahi kuzozana na Ronaldo, ni mtu mzuri sana na anapokuwa uwanjani anafanya vizuri sana na kila mmoja analijua hilo”
“watu muda mwingine wanapenda kupotosha mambo, hatujawahi kuingia katika mgogoro” alisema Bale.

Bale na Ronaldo wote wanafahamika kwa ufundi wao wa kupiga mipira ya adhabu (free kick) na Bale alisema alipata Ujuzi huo kupitia mafunzo ya pamoja na Ronaldo.


“Inafahamika wazi kuwa mipira ya adhabu ya upande wa kushoto ni ya Ronaldo na mipira ya adhabu ya upande wa kulia ni ya kwangu katika kila mchezo. Hivyo tunajua kisawasawa nini tunakifanya” aliongeza Bale ambae juzi ameisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa goli 3 -2 dhidi ya Rayo Vallecano, mechi ambayo Ronaldo hakucheza kutokana na maumivu ya msuli.


Bale, Benzema na Christiano Ronaldo wamepewa jina la BBC kutokana na uwezo wao wa ufungaji katika klabu ya Madrid



Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com 

0 comments:

Post a Comment