Monday, April 25, 2016

Riyad Mahrez Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwaka EPL


Staa wa Leicester City Riyad Mahrez ametangazwa jumapili hii kuwa mchezaji bora wa mwaka wa ligi ya Uingereza baada ya kupigiwa kura na wachezaji wenzie.
Mahrez akiwa na tuzo yake

Mahrez (25) aliyezaliwa Ufaransa na kukulia Algeria amepokea tuzo hiyo katika sherehe zilizofanyika jijini London.

Mchezaji wa Tottenham Dele Alli alitwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa mwaka katika tuzo hizo zilizotolewa na Proffessional Footballers’ Association (PFA).

Mahrez aliyejiunga na Leicester akitokea ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 mwaka 2014 ameifungia Leicester magoli 17 na kutoa pasi za magoli (Assists) 11 katika kuisaidia timu yake inayotegemewa na wengi kuchukua ubingwa wa EPL msimu huu.
Delle Alli 

“Shukrani zote ziende kwa wachezaji wenzangu” alisema Mahrez. “Na kwa kocha wangu na Staff nzima ya timu, bila wao nisingepata hii tuzo na nisingeweza kufunga magoli uwanjani, haya ni matunda ya umoja wa timu na napenda kuchukua tuzo hii kwa niaba yao” aliongeza Mahrez ambae jana pia ameisaidia timu yake kuondoka na ushindi wa goli 4 – 0 dhidi ya Swansea huku yeye akifunga goli la kwanza la mchezo.











pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com 

0 comments:

Post a Comment