Monday, April 25, 2016

Samatta Anusurika Kuvunjika Pua



Taarifa mbaya kuhusu star wa Bongo kwenye ligi ya Ubelgiji Mbwana Samatta ni kwamba, amepata majeraha katika mchezo wa Jumapili April 24 usiku ambapo Genk ilishuka dimbani, mchezo  ambao alianza kwenye kikosi cha kwanza lakini hakuweza kumaliza dakika zote 90.

Samatta hakuweza kumalizia kipindi cha pili baada ya kupata maumivu katika kipindi cha kwanza baada ya kugongwa pua. Nafasi yake ilichukuliwa na Nikolaos Karelis aliyeingia dakika ya 46 kipindi cha pili.
Genk ilipoteza mchezo huo kwa kukubali kipigo cha magoli 2 - 1



Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment