Mbrazil Neymar ni Mchezaji wa karibuni zaidi Mkataba wake kuvuja akiwa Barcelona baada ya Mtandao wa Football Leaks kuweka wazi mkataba wake mpya Camp Nou. Mchezaji huyo alihamia Barcelona akitokea Santos ya Nchini Brazil akisaini dili la miaka mitano mapema mwezi wa sita mwaka 2013 na baba yake akisemwa kuwa ndo mwakilishi wake katika dili hilo.
Mkataba huo unaonyesha thamani ya Mshahara ambao Neymar anapokea kwa mwaka ambao ni Euro milioni 5 achilia mbali bonasi mbalimbali zinazomfanya Mchezaji huyo wa kibrazil kujikusanyia zaidi ya Euro Million 49.5 katika kipindi chake chote cha Mkataba.
Neymar amekuwa na Mchango mkubwa sana katika klabu ya Barcelona akishirikiana vizuri na Messi na Suarez akiwa ameshafunga magoli 21 hadi sasa katika La Liga msimu wa 2015/2016.
0 comments:
Post a Comment