Timu ya Simba inajiandaa kupambana na Coastal Union ya
Jijini Tanga leo Jumatatu katika Uwanja wa Taifa Dar es salaam, Kocha wa timu hiyo
Jackson Mayanja amesema timu iko fiti wamejiandaa vizuri na wanatarajia ushindi
katika mechi ya leo
.
Coastal na Simba zitamenyana kwenye mchezo wa Kombe la FA
katika hatua ya robo fainali, wakiwa wanawania kuingia hatua ya nusu fainali
huku timu za Yanga, Azam na Mwadui zikiwa tayari zimeshaingia katika hatua
hiyo.
“Nimejiandaa vyema na kikosi changu kuelekea mechi yetu na
Coastal, tunahitaji kushinda mchezo huo ili kuweza kufanikiwa kuingia hatua inayofuata
.
“Nashukuru wachezaji wangu wapo vyema na Kiiza na Juuko
tayari wamesharejea kikosini na wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo
huo,” alisema Mayanja.
0 comments:
Post a Comment