Mashabiki wa Yanga wameshindwa kuvumilia kinachoendelea kwa
sasa katika timu yao hali iliyochangiwa pia na sare ya Juzi dhidi ya Al Ahly.
Hali hiyo imepelekea Mashabiki hao kumfuata Kocha Charles Boniface Mkwasa anaeitumikia
timu ya Taifa wakimwomba arejee kikosini kwa kile wanachodai mashabiki kuwa
timu hiyo kwa sasa ni kama inapoteza muelekeo.
Mashabiki hao
walimzingira Mkwasa akijiandaa kuondoka uwanja wa taifa juzi katika pambano la
Yanga. Licha ya Mkwasa kujitahidi kuwatuliza mashabiki hao lakini bado
walikuwa wakipaza sauti zao zikizodhihirisha wazi kuwa wanamuhitaji mkwassa
arudi nyumbani kwa maana ya Yanga huku wakiamini kabisa kuwa kurudi kwake Yanga
kutaisaidia klabu hiyo kufanya vizuri zaidi tofauti na hali ilivyo kwa sasa.
“Sisi mashabiki wa Yanga, tunakuambia urejee kikosini,
tunakuhitaji zaidi huku kuliko timu ya taifa.
Timu kwa sasa hatuielewi, haina stamina hata mabao mengi
tuliyokuwa tukifunga kipindi ulipokuwepo hakuna tena, kwanza TFF kwenyewe
hapaeleweki. Rudi nyumbani tu,” yalisikika maneno hayo kutoka kwa mmoja wa
mashabiki waliokuwa wamemzingira Kocha huyo wa Timu ya Taifa.
Mkwasa aliondoka Yanga baada ya kupewa ofa ya kuifundisha
timu ya Tanzania Taifa Stars.
0 comments:
Post a Comment