Kiungo wao mchezeshaji Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amepona malaria na tayari ameanza mazoezi.
Kiungo huyo, hivi karibuni alizuiwa kuingia kwenye kambi ya maandalizi huko Pemba katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly iliyochezwa juzi Jumamosi na matokeo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mnyarwanda huyo, pia aliukosa mchezo huo wa Al Ahly kutokana na adhabu ya kadi mbili za njano alizozipata katika mechi dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius na APR ya Rwanda.
Niyonzima alisema juzi Jumamosi alianza mazoezi mepesi ya binafsi kwa kukimbia mbio ndefu na fupi kwa ajili ya kujiweka fiti.
Niyonzima alisema, amepanga kujiunga na wenzake katika mazoezi ya pamoja ya timu leo Jumatatu kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Al Ahly itakayopigwa huko Misri.
“Mashabiki waondoe hofu na wanachotakiwa ni kuwa na matumaini makubwa ya kufanya vema katika mechi ijayo ya marudiano dhidi ya Al Ahly ambayo ninaamini tutapata matokeo mazuri.
“Mimi nimepona malaria, nashukuru nimeanza mazoezi mepesi ya binafsi kwa ajili ya kujiweka fiti zaidi baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki moja, hivyo mechi ijayo nitakuwepo uwanjani,” alisema Niyonzima.
0 comments:
Post a Comment