WINGA machachari wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Farid Mussa, amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa walichofanya jana walipoichapa Esperance ya Tunisia mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Farid, 19, alikuwa katika kiwango bora jana akifunga bao la kusawazisha dakika ya 69 lililowarudisha mchezoni Azam FC na kupata bao la ushindi ndani ya dakika moja lililofungwa na Ramadhan Singano ‘Messi’ dakika ya 70.
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Farid alisema kuwa haikuwa kazi rahisi na wamepambana kinoma kutokana na Esperance kuwa na uzoefu mkubwa kwenye michuano hiyo na pia ukizingatia wamewaacha mbali kisoka.
“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kucheza vema leo (jana) na kuifungia bao timu yangu, haikuwa kazi rahisi kufanya hivyo tumepambana sana hadi kupata matokeo hayo,” alisema.
Azam FC ina nafasi Tunis
Farid alizungumzia pia mchezo wa marudiano utakaofanyika Aprili 20 mwaka huu jijini Tunisia na kudai kuwa wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri ugenini.
“Bado nina uhakika wa asilimia 100 kwa Azam FC kufanya vizuri ugenini, na hii itawezekana kama watu watajituma kama tulivyojituma hapa kipindi cha pili, vilevile kupeana moyo naamini tutafanikiwa,” alisema.
Chanzo: Azamfc Official Site
Monday, April 11, 2016
"Haikuwa Kazi Rahisi, Tumepambana Kinoma" Farid
Related Posts:
TWIGA STARS KUVAANA NA RWANDA Timu ya soka Taifa ya Wanawake ya Tanzania – Twiga Stars, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Rwanda, utakaofanyika Uwanja wa Amahoro jijini Kigali, Rwanda. Rwanda wameomba mchezo ufanyike ili ku… Read More
PAUL NONGA ANYOOSHA MIKONO YANGA Mchezaji aliyejiunga na Yanga akitokea Stand United Paul Nonga amesema ameuomba uongozi wa Yanga umuuze. Nonga amefikia uamuzi huo baada ya kukosa nafasi ya kucheza muda mwingi katika klabu hiyo. ”Nimeomba kuuzwa na tay… Read More
AL AHLY WAMNYATIA DONALD NGOMA Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Donald Ngoma ameanza kuwindwana vigogo wa soka la Misri na Afria timu ya Al Ahly. Ngoma amekuwa mshambuliaji tishio sana katika klabu ya Yanga na ametoa mchango mkubwa sana katika ma… Read More
MUNAODHANI KIPRE TCHETCHE ATAJIUNGA NA YANGA, HII NDO KAULI YAKE KWENU Mchezaji Kipre Herman Tchetche amesema hana mpango wa kujiunga na klabu nyingine yoyote ya Tanzania. Tchetche amefikia hatua ya kuyazungumza hayo kufuatia uvumi unaotawala hivi sasa ukimuhusisha yeye kujiunga na klabu ya… Read More
KIPRE TCHETCHE AOMBA KUONDOKA AZAM FC Kipre Tchetche mchezaji wa Azam FC raia wa Ivory Coast amesema inatosha sasa kucheza Tanzania hivyo anataka kwenda kujaribu sehemu nyingine. Kipre ambaye ana mwaka mmoja umebaki katika mkataba wake ametosheka na muda ali… Read More
0 comments:
Post a Comment