Sunday, May 1, 2016

MBIO ZA UBINGWA LA LIGA ZAZIDI KUWA NGUMU


Barcelona inazidi kubaki kileleni kwa tofauti tu ya magoli na Atletico huku zikiwa zimebaki mechi mbili tu kumaliza msimu baada ya ushindi wao wa jana wa 2 – 0 magoli yaliyofungwa na Rakitic na Luis Suarez dhidi ya Real Betis.

Siku ya jana iliyokuwa na presha kubwa kwa timu zote tatu (Real Madrid, Atletico na Barcelona) kushuka uwanjani, ilishuhudiwa timu hizo zote zikiibuka na ushindi katika mechi zao. Na kuifanya Barca kuendelea kubaki kileleni kwa pointi sawa na Atletico Madrid huku Real Madrid ikiwa pointi moja nyuma ya Atletico na Barcelona.

Antonio Griezmann alitokea Bench na kufunga goli hilo la pekee na la ushindi, Atletico ilipoibuka na ushindi wa goli 1 – 0 dhidi ya Rayo Vallecano.
Goli la Gareth Bale lilitosha kuipa ushindi Real Madrid katika mchezo wao uliopigwa hapo jana dhidi ya Real Sociedad.

Barca wanahitaji kushinda mechi zao mbili zilizobaki, mechi moja wakicheza nyumbani dhidi ya Espanyol na moja ya Ugenini dhidi ya Granada ili kujihakikishia kuutwaa ubingwa huo.

“Sidhani kama Wawili hao (Atletico, Real Madrid) kuna atakaekubali kupoteza pointi katika michezo yao, hivyo tunatakiwa kushinda mechi zetu zote” alisema Bosi huyo wa Barcelona Luis Enrique

Katika mchezo wao Barcelona dhidi ya Real Betis, Beki Heiko Westermann wa Betis alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza baada ya kumchezea rafu mbaya Rakitic, hivyo kupewa kadi ya njano ya pili.

Short La Liga
Standings

#
Team
GP
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Barcelona
36
27
4
5
104
29
75
85
2
Atlético Madrid
36
27
4
5
60
16
44
85
3
Real Madrid
36
26
6
4
105
32
73
84
4
Villarreal
35
17
10
8
42
31
11
61
5
Celta Vigo
35
16
9
10
49
55
-6
57



Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment