Sunday, May 1, 2016

BORUSSIA M’GLADBACH WAHARIBU SHEREHE ZA UBINGWA WA BAYERN MUCHEN


Vijana wa Pep Guardiola walizuiwa kusherehekea ushindi wao wa 4 Mfululizo baada ya kulazimishwa sare na Borussia Monchengladbach, mchezo uliopigwa katika uwanja wa Allianz Arena jana.

Andre Hahn alisitisha sherehe za ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya 4 Mfululizo baada ya kuisawazishia timu yake goli dakika ya 72, baada ya Thomas Muller kuifungia Bayern goli dakika ya 6’ ya mchezo. Bayern endapo wangeshinda mechi hiyo wangetawazwa rasmi mabingwa wapya wa Bundesliga msimu 2015/2016,  hivyo watatakiwa kusubiri wiki moja baadae katika mchezo wao na Ingolstadt utakaopigwa siku ya May 7 ambapo wakishinda watakuwa mabingwa tena kwa mara ya 4.

Kwa sasa wako mbele kwa tofauti ya pointi 5 na Borussia Dortmund ambao wameibuka na ushindi wa magoli 5 – 1 dhidi ya Wolfsburg hiyo hiyo jana.




Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment