Sunday, May 1, 2016

UJUMBE WA PAUL POGBA KWA MASHABIKI WA SOKA DUNIANI


Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba amekuwa ni miongoni mwa ma Midfielders wazuri zaidi duniani tangu ajiunge na vigogo wa Italia Juventus.
Superstaa huyo wa Juve na timu ya Taifa ya Ufaransa anaamini atayafikia mafanikio makubwa katika Career yake hiyo kama Pele na Diego Maradona.

Baada ya kuachwa na Man United mwaka 2012 Pogba amekuwa ni Midfielder bora zaidi barani Ulaya, huku vilabu vingi Barani humo vikionyesha kumuhitaji Nyota huyo vikiwemo Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich.

Mfaransa huyo mwenye miaka 23 kwa sasa ameshinda mataji 4 ya Serie A na kombe la Copa Iitalia akiwa pia ni miongoni mwa wachezaji wa Juve waliocheza fainali ya Uefa Champions mwaka 2015 na kufungwa na  Barcelona. Lakini kwa sasa Pogba amekuwa na matarajio makubwa zaidi na kusema ni matumaini yake kuwa  atakuwa miongoni mwa wachezaji bora zaidi Ulimwenguni katika historia ya Mpira wa miguu.

“Nataka kuwa Legend kama Pele au Maradona” alisema Pogba alipozungumza na Gazeti la La Repubblica.

“Au hata zaidi ya hao, sio kwamba nasema mimi ni bora zaidi, ni kwamba nataka niwe bora zaidi” aliongeza Pogba.

“Nina tatizo moja, Nachukia kushindwa, na napenda kuwa tofauti na wengine, nataka kufanya vitu ambavyo hakuna aliewahi kuvifanya. Najituma kwasababu nina lengo la kuwa bora na ni kwa sababu nafurahi pale ninaposhinda” alisema Pogba

“Naweza nisiwe miongoni mwa wachezaji wanaopendwa sana, lakini hilo sio lengo langu, najitahidi ili nije kuwa bora”.



Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment